Kampuni ya Netflix imesimamisha mpango wa Utengenezaji wa filamu ya Will Smith ‘Fast And Loose’ kufuatia sakata lake la kumchapa kibao mchekeshaji Chris Rock kwenye usiku wa Tuzo za Oscars.
Kampuni ya Netflix imesimamisha mpango wa Utengenezaji wa filamu ya Will Smith ‘Fast And Loose’ kufuatia sakata lake la kumchapa kibao mchekeshaji Chris Rock kwenye usiku wa Tuzo za Oscars. Tovuti mbali mbali zinaeleza kwamba, filamu hiyo ilianza kukosa muelekeo baada ya kumpoteza Muongozaji wake, na wakati Netflix wakiwa kwenye mihangaiko ya kutafuta mtu mwingine, ndipo sakata la Will Smith likaibuka na kuwafanya wautie kwapani mpango huo.