Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye West kupiga hela filamu ya maisha yake

Kanye West Danny Mcbride Movie 1 Danny McBride na Kanye West

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jicho la rapa na mjasiriamali nyota kutoka nchini Marekani Kanye West kwa sasa linautazama upande mwingine wa fursa za kutengeneza pesa kupitia historia ya maisha yake.

Inaelezwa kuwa Kanye ametuma maombi kwa mwigizaji mahiri wa nchini Marekani Danny McBride akimtaka kuchukua nafasi yake na kuuvaa uhusika wa Kanye West kwenye filamu anayotarajia kuanza kuishughulikia siku za usoni, itakayokuwa imejikita zaidi katika kuelezea kwa undani historia nzima ya maisha ya nyota huyo, mihangaiko,mapito, misukosuko mpaka mafanikio.

Taarifa hiyo imetolewa na mwigizaji McBride alipokuwa kwenye mazungumzo na Jimmy Kimmel ambapo aliweka wazi kila kitu alichozungumza na Kanye West kuhusu mkakati huo.

Bride amesema alipokea simu kutoka kwa Kanye West akimtaka kuhusika kwenye filamu hiyo huku akidhihirisha wazi kuwa amelipokea kwa mikono miwili ombi la Kanye na kusema yuko tayari kuingia location kwa ajili ya kutengeneza filamu hiyo.

Bride ni mchekeshaji na muigizaji mahiri aliyewahi kufanya vizuri zaidi kwenye filamu nyingi ikiwamo Good Vibes, The heartbreak kid pamoja na 30 minutes or less.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: