Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Will Smith aenda kuombewa India

Smith India Will Smith aenda kuombewa India

Mon, 25 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Will Smith ameonekana na kupigwa picha kwa mara ya kwanza toka tukio la Machi 27, mwaka huu la kumpiga kofi Chris Rock kwenye tuzo za Oscar, Smith alifika na kuondoka Mumbai, India wiki hii iliyopita.

Mapaparazi India wamedai alikuwa na kazi za Kifilamu au alikuja India kwaajili ya mapumziko ya kiroho, “Amekuja India ili kupata ushauri wa kiroho na jinsi ya Kudhibiti na kumudu hasira zake".

Will Smith ameshaondoka India, hivi karibuni palikuwa na ripoti kuwa amezidi kupata ofa kubwa za filamu baada ya drama za Oscar na Chris Rock.

Mpaka sasa Chris Rock hajapata ofa au dili kubwa lenye pesa ya kutosha ya kumfanya afunguke kuhusu tukio hilo kama alivyosema kuwa hatofunguka mpaka alipwe mkwanja mrefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: