Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama wa Will Smith: Ndiyo mara yangu ya kwanza kumwona amekasirika

Will  Smith Carolyn Smith Mama wa Will Smith: Ndiyo mara yangu ya kwanza kumwona amekasirika

Wed, 30 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Carolyn Smith, mamake Will Smith, amesema walikuwa wamekusanyika pamoja na familia nyumbani kwake viungani mwa Philadelphia Jumapili usiku, akifurahi kumtazama mwanawe kwenye tuzo za Academy.

Alikuwa na furaha kupindukia baada ya mwanawe mwigizaji kupata tuzo yake ya kwanza ya Oscar lakini alishtushka baada ya kumuona Will Smith akimpiga mchekeshaji Chris Rock.

"Yeye ni mtu mwenye anayependa usawa," alisema. "Ndiyo mara ya kwanza nimewahi kumuona akiwa na hasira kiasi hiki. Mara ya kwanza katika maisha yake."

Nyota huyo aligonga mwamba baada ya kufanya mzaha kuhusu mke wa Smith, Jada Pinkett Smith aliyenyolewa kichwa.

Ellen Smith, dadake Will Smith, alizungumza na kituo hicho kuhusu shinikizo analopitia kaka yake kama mtu mashuhuri.

"Kila mtu ameonewa au kunyanyaswa kwa namna fulani," alisema. Ninaelewa kabisa."

Carolyn Smith alisema ushindi wa mwanawe siku ya Jumapili ulikuwa kilele cha miaka ya matumaini na bidii ya mwigizaji huyo.

"Nimekuwa nikingoja na kusubiri na kusubiri, alisema. Niliposikia jina, nilikuwa tu nasema, Ndiyo!"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: