Mama mzazi wa Chris Rock ameongea kuhusu tukio la mtoto wake kupigwa kofi na mwigizaji maarufu, Will Smith wakati wa shoo ya Tuzo za Oscar mwaka huu.
"Smith alipompiga kofi Chris, ni kama ametupiga kofi wote, lakini zaidi ni kama amenipiga kofi mimi, unapomuumiza mtoto wangu, unaniumiza mimi".
Mama Chris aliongezea kuwa, “Smith alivyompiga mwanae kisa kupewa jicho la hasira na mke wake, je angekamatwa na polisi, je mwanae angepata madhara zaidi kama kuanguka. Nimefurahishwa na jinsi mtoto wangu alivyoweza kumudu hali ile bila kuonyesha hasira," amesema mama huyo.
Mpaka sasa Chris Rock hajapata ofa au dili kubwa lenye pesa ya kutosha ya kumfanya afunguke kuhusu tukio hilo kama alivyosema kuwa hatofunguka mpaka alipwe mkwanja mrefu.