Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano Sudan yaingia wiki ya 12

Sudan 93.png Mapigano Sudan yaingia wiki ya 12

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: Voa

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na Wanajeshi wa kikosi cha RSF yaliongezeka siku ya Jumapili, wakati vita katika mji mkuu wa nchi hiyo na maeneo ya magharibi vikiingia wiki ya 12, bila dalili zozote za kumalizika kwa mzozo huo kwa amani.

Mashambulio ya anga na mizinga yalishuhudiwa, na milio ya silaha ndogo ndogo kusiskika, hasa katika mji wa Omdurman, na pia katika mji mkuu Khartoum, huku mzozo huo ukizidisha mzozo wa kibinadamu, na kutishia kuenea kuathiri maslahi mengine ya kieneo.

RSF ilisema iliangusha ndege ya kivita ya jeshi, na ndege isiyo na rubani huko Bahri, katika taarifa ambazo jeshi halikudhibitisha mara moja.

"Tunaogopa, kila siku mashambulisi yanazidi kuwa mabaya," Nahid Salah mwenye umri wa miaka 25, anayeishi kaskazini mwa Omdurman, alisema katika mahojiano ya simu na shirika la habari la Reuters.

RSF imedhibiti, kwa kiasi kikubwa, ardhi ya mji mkuu, na imeshutumiwa kwa uporaji na kuchukua nyumba kwa lazima, wakati jeshi likilenga zaidi, kufanya mashambulio ya anga na kutumia mizinga.

Chanzo: Voa
Related Articles: