Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Bandari: Watanzania wana haki ya kuzungumza – Silaa

Jerry Silaa Bg Jerry Silaa

Sat, 29 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtanzania yeyote mwenye kuona kuna eneo anahitaji lifanyiwe marekebisho kwenye mkataba wa IGA, ipo ibara inayosimamia marekebisho ambayo inaruhusu pande zote mbili kutaka wakae na wakafanya marekebisho kwani Watanzani awote wana haki ya kuzungumza.

Hayo yamebainishwa hii jana Julai 28, 2023 na Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa wakati akifanya Mahojiano na Kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Clouds na kusema Watanzania wamejitengenezea mazingira ya ya uoga na ni lazima kujiuliza kipi hatuna nchini.

Amesema, “na kama pande mbili zitakaa tena kuongeza muda wa majadiliano basi haki itabaki chini ya serikali kwa kuamua namna gani jambo hili linapaswa kutekelezwa, Watanzania wote wana haki ya kuzungumzia mkataba huu, lakini lazima tuuweke kisheria.”

Silaa ameongeza kuwa, “Tanzania tumejitengenezea mazingira ya kujiweka kwenye uoga na kuna mambo tunasema sana, tuna mbuga, tuna ardhi, tuna mlima lakini vilevile ifike wakati tujiulize hatuna nini? Hatuna nini na lenyewe ni swali.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: