Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nape acharuka: Leteni ushahidi

Waziri Nape Nape Nnauye.

Sun, 20 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewataka watanzania kupuuza madai yanayoenezwa mitandaoni kuwa amepiga simu kwa baadhi ya vyombo vya Habari na kutoa maelekezo kwa vyombo hivyo kutochapisha waraka wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) unaohusu mkataba wa Uwekezaji Bandarini kwani hakuna ukweli wowote wa tuhuma hizo.

Waziri Nape amewaonya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuzusha habari za uongo kumhusu kwamba hawatafanikiwa.

"Ninawapa changamoto hawa wanaouzusha huu uongo,walete ushahidi wa mimi kupiga simu kwa vyombo vya habari na kuvieleza nini cha kuandika na niko tayari kuwajibika wakileta ushahidi huo"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: