Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wametishia kuipindua serikali – Nape

Gdt Slaa Mwambukusi Mdude Wametishia kuipindua serikali – Nape

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini, imekanusha madai ya Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa kwamba imewakamata Watu watatu (Dkt. Wilbroad Slaa, Mdude Nyagali na Wakili Boniface Mwabukusi), kwasababu za kukosoa mkataba wa Uwekezaji wa Bandari, ikisema sio ya kweli bali Watu hao wamekamatwa kwasababu za kuitisha maandamano ya kuiondoa Serikali madarakani.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mtandao wa Twitter wa Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye imesema, hakuna aliyekamatwa na hakuna ambaye atakamatwa Tanzania kwa kukosoa mkataba wa Bandari na mradi, mpango, programu au sera yoyote kuhusu mkataba huo.

“Watuhumiwa wamekamatwa kwa kutishia kufanya maandamano ya kuiondoa Serikali madarakani, pia kuhamasisha Wananchi kuwashambulia Polisi, wamekamatwa ili kufikisha ujumbe mzito kwa Wakosoaji wanaofikiria kufanya makosa yoyote ya kijinai,” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa, “kukamatwa kwa Watu hao hakuzuii uhuru wa kutoa maoni Tanzania ila ni sehemu ya hatua za kisheria zinazolenga kuzuia maandamano yanayoweza kusababisha uasi dhidi ya Serikali iliyochaguliwa Kidemokrasia.”

“Tangu imeingia madarakani March 2021, Serikali ya Rais Samia imekuza demokrasia kwa kuondoa vikwazo vya kisiasa kwa Vyama vya Siasa ikiwemo kuruhusu mikutano ya kisisasa, kuruhusu Online TV na magazeti yaliyofungiwa kufanya kazi na kuboresha uhuru wa kujieleza,” imeeleza taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: