Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anna Tibaijuka amekosoa mkataba wa bandari hajakamatwa

Anna Tibaijuka Msd Anna Tibaijuka amekosoa mkataba wa bandari hajakamatwa

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kukamatwa kwa Dkt. Slaa, Mdude na Wakili Mwabukusi hakuhusiani na mkataba wa Bandari huku akisema wapo Watu wengi waliokosoa mkataba huo akiwemo Prof. Tibaijuka, TLS na hata wapo Watu waliofungua kesi kupinga mkataba huo lakini wote hawajakamatwa kwakuwa walikosoa kwa hekima bila kukiuka sheria.

Akiongea Jijini Arusha leo, Waziri Ndumbaro amesema “Nchi zilizoendelea Mtu kuvaa chupi na sidiria wakati wa Summer hiyo ni hekima, sasa Tanzania kufanya hivyo ni hekima?, kila Mtu atakushangaa, sasa kosa letu tunataka kutumia hekima ya kimagharibi kuileta hapa, sisi kwetu kumtukana Rais sio hekima, uchochezi haiwezi kuwa hekima, kuigawa Nchi kwa itikadi mbalimbali haiwezi kuwa umoja”

“Uhuru wa maoni sio haki pekee ya Binadamu kuna haki nyingine ambazo wakati unatekeleza uhuru wako wa maoni lazima uzingatie hizo nyingine, kuna tofauti kati ya kauli za kukosoa na kauli zinazovunja haki za wengine, kutukana Viongozi na kauli zako zikileta makosa ya jinai uhuru wako unaishia hapo na tutaanza kukushughulikia.

“Kukamatwa kwa Dkt. Slaa, Mwabukusi na Mdude hakuhusiani na mkataba wa Bandari, kuna Watu walikosoa sana mkataba ule na mmoja ni Prof.Tibaijuka hivi amekamatwa?, na hata juzi alihojiwa na Vyombo vya Habari vya Kimataifa akaendelea kukosoa, ila amekosoa bila kukiuka sheria yoyote.

“TLS walitoa waraka wao kukosoa, Sungusia ndiye anaongoza TLS na yupo hapa, Sungusia wewe ulikamatwa?, waliofungua kesi ya Bandari kule Mbeya ambao wameiburuza Serikali Mahakamani hakuna aliyekamatwa,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: