Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tukisema tusiambiwe tunachanganya Dini na Siasa - Shoo

Shoo Pic Baskofu Askofu Dkt. Fredrick Shoo.

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Fredrick Shoo amesema Kanisa hilo linaunga mkono fursa zinazotengeneza kuwawezesha Wananchi kupata maendeleo kupitia Utawala wa Sheria, Kuheshimu Haki za Binadamu na kuruhusu Demokrasia ya kweli kwa Wananchi na kwenye Vyama vya Siasa

Askofu Shoo ameyasema hayo jana Agosti 21 katika maadhimisho ya miaka 60 ya kanisa hilo yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Makumira, mkoani Arusha.

"Viongozi wa Dini zote kwa uwakilishi tuliomba kuja kukuona (Rais Samia) mwanzoni mwa jambo hili, kwa ungwana ukatupokea na tukakukabidhi maoni yetu na ukaahidi utayawasilisha kwa wataalam kufanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.

"Lipo hili la DP World Mheshimiwa…kwanza naomba ieleweke wazi Kanisa linaunga mkono uwekezaji, hatupingingi uwekezaji na tunajua wewe kwenye nia yako unataka uwekezaji, hata hivyo jambo hilo limekuwa na maoni mbalimbali ya wananchi na vyombo vya habari.

"Lakini Mheshimiwa Rais tunatambua kwamba sisi viongozi wa dini zote tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni na ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama viongozi wakuu wa dini, ukaahidi kuwa maoni yatafanyiwa kazi, tuna imani na wewe

Ninatambua kuwa ulipokea kijiti katika mazingira magumu sana, lakini pia pamoja na mazingira yale wewe ukaanza historia mpya ya nchi yetu ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Urais, kuna wengi hawakuamini, hawakutaki na mpaka leo wamebaki na jinamizi la namna hii, huu ulikuwa ni mpango wa Mungu

“Kama tukiona kuna sehemu hakupo sawa hatutaacha kuwaona, kuwashauri, kukemea na ikifika hatua hiyo tusiambiwe kuwa tunachanganya Dini na Siasa.”

"Najua katika jambo hilo linaelekea mahali tunataka kugawanyika kabisa, wengine wanatumia sababu za kidini, wengine wana maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi, nashukuru Mungu amekujalia hekima kama mama na kiongozi, umekaa kimya

"Mimi nilikerwa juzi niliposikia baada ya mtu mmoja ..akisema kwanini Serikali inatumia pesa zake kusaidia au kuendesha taasisi za wakristo, ...watu wamesahau historia, kwenye miaka ile ya 90 kuelekea 2000.

"Kanisa la Kilutheri Tanzania kwa kushirikiana na marafiki zake wa nje na ndani ya nchi, tuliongoza kampeni kubwa ya Tanzania kufutiwa madeni na nchi za G7...na Tanzania ikafutiwa madeni...Tuheshimu jambo hilo. Kwahiyo naomba sana mtu asibeze au kudhihaki ushirikiano huu kwa sababu yoyote ile.

"Umoja wa Taifa letu la Tanzania, mshikamano ni muhimu kuliko Mtu au kundi lolote, niwaombe Viongozi wenzangu wa Dini zote, niwaombe Wanasiasa, kuacha kabisa kujaribu kuwagawa Watu kwa misingi ya Dini au kwa misingi ya itikadi iwayo yoyote ya kisiasa na kwa misingi ya maslahi binafsi.

"Niombe Serikali yako kukataa na kukemea kwa nguvu yote wale wote wanaoonesha dalili za kutugawa kwa utofauti wa Dini zetu, hata pale Mtu anaposema jambo la kuipendeza Serikali iwapo amejenga hoja yake katika msingi wa kutugawa kidini au kwasababu nyingine yoyote huyo akemewe, tumkatae hana nia njema," alisema Shoo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: