Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo: Suala la bandari si la mtu mmoja, ni la CCM

Chongolo Aitaka Wizara Ya Fedha Kurejesha Fedha Ilizochukua Hospitali Ya Bahi Daniel Chongolo

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka Watanzania wasikubali kupotoshwa kuhusu mkataba wa uwekezaji bandarini kwa sababu utakuwa na manufaa mengi ta Taifa.

 Amesema mkataba huo ni wa CCM sio mtu mmoja na amesisitiza kuwa suala hilo lipo kwenye ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020, ibara ya 59 na ukurasa wa 92 kuhusu uboreshaji wa bandari.

Chongolo amesema hayo leo Julai 15, 2026 wakati akihutibia wananchi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Ruanda Nzovwe, jijini Mbeya.

Amesema kuna watu wametengeneza uongo ili kusapoti dhamira ya kupotosha uboreshaji wa bandari nchini.

“Serikali imepewa msukumo na chama kinasimamia kuhakikisha utekelezaji unafanyika, naagiza Serikali ichakate haraka kuelekea kwenye mkataba wa uwekezaji wa bandari,” amesema Chongolo na kuongeza.

“Kazi ya maneno ya siasa ni ya wanasiasa, watendaji wasihangaike kujibu. Eti jambo la fulani hata angekuwa nani ndani ya CCM, agenda isiyo na maslahi ya watu haitapita.”

Amesema ilani hiyo ya CCM ndiyo iliyoweka ahadi ya kuboresha bandari zote nchini.

“Aliyeandaa ilani ndiye aliyeweka haya malengo, mjadala wa ilani ulianza mwaka 2020. Tuliahidi, baada kuahidi tunatekeleza. Tukicheka na wanaopotosha adhabu itakuwa kwetu,” amesema Chongolo.

Amesema CCM itakusanya maoni ya wananchi na yale yenye tija yatafanyiwa kazi.

Kwa mujibu wa Chongolo, takwimu zinaonyesha kuwa bandari kwa sasa inaingiza zaidi ya Sh7 trilioni huku asilimia 99 ya fedha hizo ikitumika kwa matumizi yao wenyewe.

“Nani anakula hizo Sh7 trilioni? Sasa wakiambiwa ulaji unakatwa watafunga midomo? Kuna genge la watu wana mlo na hawataki kuona mambo yanabadilika,” amesema na kuongeza;

“CCM tuna akili timamu na habari yao wataipata, tija ikipatikana. Msikubali, msiyumbishwe agenda ni ya CCM sio ya mtu.”

Chongolo amesema hawezi kusimama na kutetea jambo ambalo haoni tija kwa Watanzania.

Amesema ikiwa kuna mwana CCM hajasimama kupigania suala hilo lazima kuna mashaka na uana-CCM wake na sio vinginevyo.

“Ukiona adui yako anakupigia makofi unapotaka kufanya jambo achana nalo, hatufungi breki na niagize Serikali ichakate haraka tusonge mbele,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: