Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar kutotajwa uwekezaji wa Bandari

Bandari Zenji Zanzibar kutotajwa uwekezaji wa Bandari

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema Zanzibar haipo katika makubaliano yaliyoingiwa na serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji kwenye bandari kwa sababu sheria iliyoanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inaipa jukumu kusimamia na kuendesha bandari zote za Tanzania Bara pekee.

Alisema jijini Mwanza alipokutana na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa bandari na kutoa ufafanuzi juu ya makubaliano hayo ya ushirikiano katika bandari.

Profesa Mbarawa alisema kusainiwa kumezusha maswali kwa wananchi wakihoji sababu za Zanzibar kuhusika kwenye mkataba huo.

“Zanzibar haipo kwa sababu Sheria namba 17 ya mwaka 2004 ya kuundwa TPA, inaipa jukumu la kusimamia na kuendesha bandari za Tanzania Bara, na si Zanzibar," alisema Mbarawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: