Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA waendeleza mjadala wa bandari

Mbowe, Lissu Mnyika CHADEMA waendeleza mjadala wa bandari

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika leo ameongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam na moja ya mambo aliyoyasema ni kwamba ipo haja ya mjadala mkubwa wa kitaifa kuhusu mkataba wa Bandari kuendelea kujadiliwa ili wakati wa kuhitimisha Bunge la bajeti, Serikali itoe majibu yatajayowaridhisha Wananchi kuhusu suala hilo.

“Bajeti hii ya mwaka 2023/24 imezungumzia miradi ya Bandari na Waziri wa Fedha amesema bajeti inaendeleza miradi ya kimkakati ikiwemo eneo la Bandari ya Bagamoyo na Bandari ya Dar es salaam, na uendelezaji wa Bandari ya Tanga, kwa Bagamoyo amesema hatua za ujenzi wa Bandari ya kina kirefu Bagamoyo unaendelea”

"Kwahiyo Serikali katika bajeti hii imepeleka mapendekezo ya matumizi ya fedha za Umma na za Washirika wa maendeleo katika uendelezaji wa Bandari, wakati Serikali inapeleka mapendekezo haya tayari kuna utata mkubwa kuhusu mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai"

"Ni vema jambo hili tuendelee kulijadili, najua jana umejitokeza mjadala Bungeni na baadhi ya vyombo vyenu vya habari leo vimenukuu michango ya Wabunge jana wakijadili kuhsu Bandari, kabla sijaendelea mbele niwaombe Wanahabari kwamba jambo hili la Bandari nafahamu kwamba baadhi yenu mna maelezo ya kutoliandika au kutolirusha au kutofanya lizungumzwe sasa kama linazungumzwa Bungeni na Wabunge ni haki kulizungumza nje ya Bunge”

"Pengine baadhi yenu mnaweza kuona baada ya majibu ya Waziri Mkuu hili suala halihitaji mjadala, Mimi nina mtazamo kwamba hotuba ya Waziri Mkuu na mjadala wa Wabunge viwe sababu ya kuendeleza mjadala mkubwa wa kitaifa kuhusu jambo hili ili wakati wa kuhitimisha Bunge la bajeti Serikali itoe majibu”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: