Menu ›
Habari
Tue, 8 Oct 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Klabu ya Wydad Athletic imetuma ofa ya tatu kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Yanga Sc Clement Mzize, imefahamika.
Matajiri hao kutoka ligi kuu ya Morocco wameongeza dau la usajili kufikia takribani Tsh 1.4B ambapo dau hilo linaweza kuongezeka hadi kufikia Tsh 2.1B kutegemea na makubaliano ya ziada.
Aidha klabu hiyo imeipa Yanga Sc ofa ya kufanya pre-season ya msimu ujao Morocco ambapo Wydad watagharamikia kila kitu.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: