Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu akiri uwepo wa mapungufu Bandarini

Majaliwa Amuagiza RC, RPC Wamkamate Mzazi Anayedaiwa Kumlawiti Mwanaye.jpeg Waziri Mkuu akiri uwepo wa mapungufu Bandarini

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekiri uwepo wa mapungufu katika Bandari ya Dar es Salaam na kusema pamoja na maboresho yaliyofanyika, hali ya utendaji wake imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na bandari shindani kikanda.

Majaliwa ameyasema hayo akiwa jijini Arusha na kutolea mfano kuwa wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari hiyo ya Dar es Salaam ni siku tano, ikilinganishwa na wastani siku moja na nusu kwa Bandari za Mombasa na Durban.

Amesema, udhaifu huo uliopo katika bandari hiyo unasababisha meli kusubiri muda mrefu nangani na hivyo kuongeza gharama, ambapo kwa siku moja ni takriban Dola za Marekani 25,000, sawa na takriban shilingi milioni 58 kwa siku.

“Kitendo cha meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakua shehena gatini kwa wastani wa siku tano ikilinganishwa na siku moja inayokubalika kimataifa kinasababisha meli kubwa kutokuja katika bandari ya Dar es Salaam,” amesema Waziri Mkuu.

Aidha, Majaliwa ameongeza kuwa ili kutatua changamoto za bandari zilizopo na kuongeza ufanisi katika mapato, ajira na kuchagiza sekta nyingine za kiuchumi, Serikali ilifanya maamuzi ya kutafuta wawekezaji wapya wanao endana na dhima ya Serikali.

Hata hivyo, Majaliwa amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali haitodharau maoni na ushauri wanaoutoa kuhusu maeneo yenye hofu kwenye mradi wa uwekezaji na kuwataka waendelee kuwa na imani kwani imejidhatiti kuhakikisha bandari inakuwa na ufanisi unaoendana na mahitaji ya sasa na kwa kuzingatia manufaa ya kijiografia ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: