Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulinzi mkali mahakamani uamuzi kesi ya uwekezaji bandari

Mwambukusi 1 Puc Ulinzi mkali mahakamani uamuzi kesi ya uwekezaji bandari

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Mbeya leo Jumatatu, Agosti 7, inatoa uamuzi wa kesi ya kupinga mkataba wa ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii, kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai (IGA), unaohusu uwekezaji katika Bandari za baharini na katika maziwa nchini Tanzania.

Uamuzi huo umepangwa kutolewa leo asubuhi hii na jopo la majaji watatu walioisikiliza kesi hiyo linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji Mustafa Ismail na Abdi Kagomba.

Kuelekea uamuzi huo leo hali ya ulinzi mahakamani hapa imeimarishwa tofauti na siku zote wakati kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa. Askari Polisi wenye sare na wasio na sare na wengine wakiwa na silaha wanaonekana katika Kona mbalimbali za mahakama hii kuimarisha ulinzi.

Katika kuhakikisha kuwa watu wote waliofika kusikiliza uamuzi huu wanapata fursa hiyo, Mahakama hiyo imeandaa ukumbi wa ziada ambamo watu wengine watakaa kufuatilia uamuzi huo Kwa njia ya video conference, ambamo watakuwa wanasikia na kuona kinachoendelea kutoka katika ukumbi walimo majaji kupitia kwenye televisheni.

Hivi sasa watu wameshajaa katika ukumbi ambamo.mahaka itadima uamuzi huo, na mawakili wa pande zote (walalamikaji na wa Serikali wameshachukua nafasi zao na sasa wanawasibiri majaji tu kuingia ili waanze kusoma uamuzi huo.

Namna mahakama itakavyoamua Katika uamuzi wake mahakama inatarajiwa kuamua kama mkataba huo ni halali au ni batili.

Katika kufikia hitimisho la uamuzi wake, Mahakama itajielekeza katika kujibu hoja sita zilizobainishwa na kukubaliwa na pande zote kama hoja zinazobishaniwa katika kesi hiyo.

Hoja zinazobishaniwa

Mosi: Kama kusaini, kuwasilisha bungeni na kuridhia mkataba waTanzania na Dubai kulikiuka kifungu cha 11(2) Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Raslimali na Maliasili, Sheria namba 5 ya mwaka 2017 kikisomwa sambamba na Sheria ya Mapitio na Majadiliano ya Mikataba ya Masharti Hasi, Sheria namba 6 ya mwaka 2017.

Mbili: Kama umma uliarifiwa na kupewa muda muafaka kushiriki na kutoa maoni yao kama ambavyo sheria zinataka kuhusiana na utaratibu wa kupitisha na kuridhia Mikataba.

Tatu: kama ibara ya 2(1), 4(2), 5(1), 6(2), 7(2), 8(1) (a-c), (2); 10(1) , 20(2) (a), (e) na (i) na (ii); 18, 21, 23(1) (3) na (4); 26, 27, na 30(2) za mkataba huo zinakiuka Ibara za 1, 8, 28(1) na (3) za Katiba ya Nchi.4: Kama IGA kati ya Tanzania na Dubai ni mkataba.

Nne: Kama IGA kati ya Tanzania na Dubai ni mkataba.

Tano: Kama Ibara ya 2 na 23 ya IGA inakiuka kifungu cha 25 cha Sheria za Mikataba Tanzania.

Sita: Kama IGA kati ya Tanzania na Dubai ulifuata taratibu za kisheria katika kuchagua njia ya zabuni ambao umewekwa chini ya kifungu cha 64 cha Sheria ya Manunuzi

Kwahiyo, mahakama itapaswa kujibu hoja hizo sita. Na ili kutoa majibu ya hoja hizo, itaangalia ufafanuzi wa mawakili wa pande zote jinsi walivyozielezea ama kuung Kesi hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023 imefunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya na mawakili wanne kutoka mikoa tofautofauti, Alphonce Lusako, Emmanuel Chengula, Raphael Ngonde na Frank Nyalus dhidi ya Serikali

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye ni mshahri wa Serikali kwa mauslanya kisheria, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge la Tanzania, ambaye ni mtendaji mkuu na mratibu wa shughuli za Bunge.

Katika hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023, wanasheria hao vijana wanapinga makubaliano hayo wakidai kuwa ni batili kwa kuwa masharti ya baadhi ya Ibara zake yanakiuka Sheria za Nchi za Ulinzi wa Raslimali na Maliasili za Nchi na Katiba ya Nchi.

Vile vile wanadai kwamba yanahatarisha mamlaka ya Nchi na usalama wa Taifa na kwamba yaliridhiwa na Bunge kinyume cha utaratibu bila kuwapa nafasi ya kutosha wananchi kutoa maoni yao.

Makubaliano hayo yalisainiwa Oktoba 25, 2023 na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, baada ya kupewa nguvu ya kisheria na Rais Samia Suluhu Hassan, huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, akishuhudia na yaliridhiwa na Bunge Juni 10, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: