Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA: Bandari ya Dar haiuzwi, ogopa matapeli

Bandari2 1 780x470nmnm TPA: Bandari ya Dar haiuzwi, ogopa matapeli

Wed, 7 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imewataka Watanzania kupuuza taarifa za upotoshaji zinazofanywa kwa makusudi na watu wenye nia ovu zinazodai kwamba serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai kandarasi ya uendeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka 100.

TPA imefafanua azimio la Bunge linahusu mkataba ambao serikali inaingia na serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi 12 kwa ajili ya kutoa nafasi kujadiliana kuhusu maeneo ambayo nchi hizo zinaweza kushirikiana katika uboreshaji na uendelezaji wa sekta ya bandari nchini Tanzania.

Ushirikiano wa nchi hizo mbili una lengo la kuongeza ufanisi wa huduma za bandari nchini, kukuza ajira za Watanzania na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji kwenye baadhi ya maeneo ya bandari ya Dar es Salaam, maeneo huru ya kiuchumi na viwanda.



Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: