Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yazuia maandamano ya CCM sakata la bandari

David Misime Kalynda Kamanda Misime

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Tanzania limepiga marufuku maandamano yaliyoitishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) katika Wilaya zote za Tanzania ili kuiunga mkono Serikali juu ya uwekezaji katika bandari.

Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “Julai 16, 2023 kupitia Vyombo vya Habari mbalimbali ikiwepo mitandao ya kijamii ameonekana Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) akitoa taarifa ya kuhamasisha maandamano katika Wilaya zote na wataanza na Dar es salaam July 18,2023 ili kuiunga mkono Serikali juu ya uwekezaji katika bandari, sheria ipo wazi kwa Mtu au kikundi cha Watu kinapotaka kuitisha maandamano taratibu zipi zinatakiwa kufuatwa”

“Pamoja na utaratibu huo wa kisheria, kuitisha maandamano Nchi nzima ni sawa na kutaka kuleta vurugu na hofu kwa Watanzania bila sababu yeyote ile kwani yapo majukwaa ya kuwasilisha jambo lolote lililo katika utaratibu wa kisheria bila kuhamasisha maandamano ya aina hiyo”

“Kwa msingi huo, Jeshi la Polisi linapiga marufuku maandamano hayo yasifanyike na hii ni pamoja na Watu wengine pia wenye nia kama hizo na badala yake wawasilishe hoja zao kupitia mikutano na vyombo vya habari.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: