Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya kupinga mkataba wa bandari Julai 20

Mawakili Bandari Kesi ya kupinga mkataba wa bandari Julai 20

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu kanda ya Mbeya imesogeza mbele hadi Julai 20, 2023 kesi namba 5/2023 ya Wadau wa katiba ya kuhoji uhalali wa mkataba uliosainiwa na Serikali ya Tanzania na kupitishwa na Bunge kwa kutengeneza sheria zitakazotumika kuongoza mikataba ya Ubinafsishaji wa bandari kwa kampuni ya DP World ya Dubai hadi Julai 20 mwaka huu.

Kesi hiyo ambayo imepangwa kusikiliwa na majaji wa tatu ilikuwa inasikiliwa na jaji Dustani Nduguru ambapo Wajibu Maombi (Wakili Serikali) waliomba mahakama isogeze mbele ili kupata fursa ya kukusanya vielezo vya waleta maombi baada ya mvutano wa mda mrefu Mahakama amewaaigiza wajibu na waleta maombi kuwasilisha nyaraka Julai 14 ili kesi ianze kusikilizwa mfululizo kuanzia Julai 20.

Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama kuu kanda ya Mbeya na Emmanuel Kalikenya Chengula, Alphonce Lusako, Raphael Japhet Ngonde na Frank John Nyalusi wakimshtaki mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Uchukuzi,katibu wa Wizara ya Uchukuzi na katibu wa Bunge.

Kesi hiyo inasimamiwa na mawikili wa kujitegemea Bonface Mwabukusi, Philip Mwakilima, Livino Haule na Caroline Luhungu.

Mawakili wa Serikali ni Hangi chanya Wakili wa serikali Ayoub Sanga wakili wa Serikali (SA) Kesi hiyo inasikiliwa na majaji watatu wa Mahakama Kuu.

Majaji wengine walipongiwa kusikiliza kesi ya kikatiba ni Abdi S Kagomba (mahakama Kuu Dodoma).

Akizungumza nje ya Mahakama mmoja wawalamikaje Alphonce Lusako asema amesema sababu ya kugungua kesi hiyo ni kutaka kupata tafsiri kisheria na kwamba hawapinga suala la uwekezaji lakini wanapinga baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye mkataba huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: