Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi hapa hoja nne za Serikali kesi ya Bandari

Bandari Afrika Kusini.jpeg Hizi hapa hoja nne za Serikali kesi ya Bandari

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miongoni hoja hizo, Serikali inadai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 7 (2) ya Katiba ya nchi.

Hoja ya pili ya Serikali, inadai kuwa shauri hilo kwa kufunguliwa chini ya ibara ya 108 (2) na chini ya kifungu cha 2 (3) cha Sheria ya Usimamiaji Haki na Matumizi ya Sheria (JALA), halina nguvu ya kuhoji ukiukwaji (sheria/Katika) kwa mambo yanayoangukia katika ibara ya 12 mpaka 29 za Katiba ya nchi (kuhusu wajibu na haki za msingi).

Na katika hoja ya tatu, Serikali inadai kuwa shauri hilo limefunguliwa wakati usio muafaka, ni batili na halina nguvu kwa kuwa wadai bado walikuwa na njia mbadala ya kupata haki wanazoziomba chini ya sheria za ununuzi.

Serikali inahitimisha hoja zake kwa kudai kuwa, kiapo kinachounga mkono shauri la msingi kina kasoro zisizorekebishika kwa kuwa hoja za kisheria (badala ya hoja za kiushahidi), maoni binafsi na hitimisho (kuhusu madai yao kwenye kesi), jambo ambalo inasema ni kinyume cha maelekezo ya kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: