Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yametimia! Sawadogo apewa "Thank You" Simba

IMG 4502 Sawadogo.jpeg Ismael Sawadogo

Sat, 1 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imeachana na kiungo wake, wa Kimataifa wa Burkina Faso, Hamed Ismael Sawadogo baada ya miezi sita tangu awasili kutoka Difaâ El Jadida ya Morocco.

“Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na kiungo mkabaji Ismael Sawadogo,” imesema taarifa ya Simba leo.

Hamed Ismael Sawadogo, anakuwa mchezaji wa nane kuachwa Simba baada ya kipa Beno Kakolanya, mabeki Gardiel Michael, Muivory Coast, Mohamed Ouattara, viungo Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Wanigeria, Nelson Okwa, Víctor Akpan na Mghana, Augustine Okrah.

Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: