Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wilson Oruma: Simba bado wana nafasi

Oruma X Chama Wilson Oruma: Simba bado wana nafasi

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Mashabiki wa Simba wakiwa wamevurugwa vya kutosha kuhusiana na matokeo na mienendo ya Timu yao.

Mchambuzi wa michezo kutoka Efm, Wilson Oruma anasema Simba bado wana nafasi ya kufanya kile ambacho walikipanga tangu mwanzoni mwa msimu.

Akizungumza Oruma anasema;

"Simba bado wana nafasi ya kufanikiwa, msimu huu bado wana nafasi ya kufanya vizuri ukiangalia kwenye ligi wamezidiwa alama tano na anayeongoza ligi huku wakiwa wana mchezo mmoja lakini pia kwenye Klabu Bingwa wana alama moja kwenye mchezo mmoja."

"Lakini kocha anatakiwa kuweka mambo sawa haraka iwezekanavyo ili afikie malengo waliyojiwekea Simba ndani ya msimu huu. Jambo la kwanza namna Simba wanavyoruhusu kufungwa magoli, ukiangalia ndani ya msimu huu, kwenye mechi zote za michuano ukiondoa ile ya Ngao ya Jamii, hajaruhusu kufungwa kwenye mechi mbili tu.

Hiyo inamaanisha ili Simba washinde mechi basi ni lazima wafunge magoli kuanzia mawili kwa kuwa wanaruhusu kufungwa magoli kwenye mechi nyingi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: