Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wilson Oruma: Mo Dewji akawaulize RITA mchakato umkomea wapi

MO Dewji: Simba Hatukati Tamaa Mohammed Dewji.

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya michezo kutoka kituo cha radio cha wa EFM, Wilson Oruma ameonyesha kushangazwa na kauli ya mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji kudai kuwa anatakatishwa tamaa kutokana na mchakato wa mabadiliko wa klabu hiyo kusimama kwa miaka sita sasa.

Oruma amedai kuwa kwa hadhi ya Mo Dewji hakupaswa kulalamika mitandaoni na badala yake angeweza kwenda kwenye mamlaka husika na kuuliza ili apate majibu kwa nini mchakato huo umekwama ili aone namna ya kukamilisha taratibu.

"Kwanza kabisa naandika haya nikiwa nafahamu hakuna mafanikio ya Simba Sports Club bila, Mohamed Dewji Mo. Mtu yeyote anayekwambia kinyume na hivi mpuuze kwa sababu wote hapa tunafahamu ni wapi, Mohamed Dewji ameitoa Simba Sc.

"Juzi tunasherehekea Simba Sc kuwa kwenye nafasi ya (7) kwa ubora barani Africa, hatua hii imefikiwa kwa sababu ya uthabiti wa Mnyama Simba Sc ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

"Hakuna kitu kingewezekana hapa bila uwekezaji wa hali na mali ya Mohamed Dewji Mo, lakini kwa masikitiko makubwa yeye mwenyewe ndio amenifikisha hapa.

"Amenifikisha kwenye hatua ya kuwaza kuwa yeye pia ni sehemu ya watu wanaokwamisha mchakato wa mabadiliko Simba Sc, kwa nini?

"Kwa sababu Mo anafahamu mchakato wa mabadiliko wa Simba SC umekwamia RITA. Hatua zote muhimu wamezivuka ikiwemo kule kwenye Fair Competition (FCC) BRELA na kwingineko.

"Mchakato wa RITA ni kuhuisha mali kutoka SIMBA SC kwenda SIMBA SPORTS CLUB LIMITED. Simba walihitajika kupeleka watu kwenye bodi ya wadhamini kwa uhakiki walifanya. Kujua Assets na Liabilities tayari. Kulihitajika pia idadi ya wanachama ambao wamekutwa na mchakato wa mabadiliko.

"Kwa nafasi ya Mo anaweza kufanya cross checking na watu wa RITA kuwauliza huu mchakato upo hapo kwa muda mrefu, sasa tatizo nini? Ana uwezo wa kufikia hata hao maboss wa RITA ikibidi. Kwa nini hafanyi hivyo unakuja kuleta TAHARUKI na sentensi (2) za Twitter?

"Simba Sc ipo kwenye kipindi muhimu cha maandalizi ya msimu baada ya kuwa na misimu hii miwili mibovu, kulikuwa na haja kweli ya Tweet ya aina hii ambayo inaleta taharuki? Au boss na wewe umemiss kuongelewa? Tajiri unataka KUTREND baba?

"Na tumkumbushe Mo Dewji kwamba huu mchakato ukishamalizika RITA unarejea kwake. Anatakiwa kutoa jina lake kwenye ile BOND ya Tsh 20 BILLION likae jina la Simba Sc pale. Sasa hivi ni kama ile Tsh 20 BILLION ni ya kwake tu ingawa anatoa gawio la 1.7 Bilioni kwa mwaka.

"Na get me Whrong hapa. Sisemi kwamba Mo Dewji hana hoja, anayo. Shida nafikiri ni TIMING na hajaitoa kupitia platform sahihi. Yaani kama yeye analalamika na Mgalilaya afanye nini? Agnes afanye nini?," amesema Wilson Oruma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: