Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WhatsApp ndio waliiomba Simba kufungua channel - CEO Kajula

Simba Channel Haji Manara

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Klabu ya Simba, Imani Kajula amesema WhatsApp waliifata Simba na kuiomba iwe timu ya kwanza Afrika Mashariki kufungua Channel ya WhatsApp.

Simba imezindua na kutambulisha hii leo channel mpya kupitia mtandao wa WhatsApp na imetambulishwa na CEO huyo kwa ajili ya kuwaweka pamoja mashabiki na kurahisisha upatikanaji wa taarifa rasmi za klabu.

"Leo tunazindua Simba Sports Club WhatsApp channel. WhatsApp imepakuliwa na watu Bilioni 2.2 duniani ndio mtandao umepakuliwa zaidi duniani. WhatsApp wenyewe walitufata kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na chaneli hii.

"Ni timu chache kama Kaizer Chiefs, Al Ahly, Barcelona, Real Madrid na Simba tumejiunga. Katika kuijaribu kabla ya kuzindua ndani ya wiki tumepata wafuasi laki moja. Faida kubwa ni mashabiki kupata taarifa na wadhamini wetu kuonyesha bidhaa zao.

"Instagram tuna watu zaidi ya 5.5 milioni, Facebook zaidi ya 1.9 milioni, Twitter zaidi ya 1.5 milioni, YouTube tukiwa na zaidi ya 438k, kwenye app imepakuliwa zaidi ya laki saba na hivi karibuni tumeshinda tuzo ya mashabiki bora," amesema Imani Kajula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: