Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazungu wamfuata Baleke Simba amefunga mabao nane

Jean Baleke Tatu Wazungu wamfuata Baleke Simba amefunga mabao nane

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi unaomsimamia Jean Baleke umeweka wazi kuwa umepokea ofa kutoka kwa timu nyingi zikiwemo zinazocheza katika ligi mbalimbali barani Ulaya.

Jean Baleke ambaye anakipiga katika klabu ya Simba kwa mkopo akitokea TP Mazembe amekuwa akifanya vyema ndani ya Simba tangu atue amefunga mabao nane katika mechi nane alizocheza kwenye ligi jambo ambalo mashabiki wengi wamekubali uwezo wake.

Akizungumza nasi, Faustino Mkandila ambaye ni moja kati ya wasimamizi waliomleta Simba mchezaji huyo ameweka wazi kuwa juu ya timu kutoka Ulaya zikiwa zinamhitaji mchezaji huyo kupitia dirisha kubwa jambo ambalo lazima Simba wafanye kazi kubwa kumbakisha mshambuliaji huyo.

“Baleke yupo Simba kwa mkopo hivyo Simba wanatakiwa kufanya kazi kubwa sana kumbakisha Baleke kutokana na timu nyingi kumnyatia haswa kutoka Afrika na Ulaya.

“Tayari timu nyingi zimeleta ofa ya kumhitaji Baleke hadi timu kutoka ligi za Ulaya wameonekana kuvutiwa na uwezo ambao ameuonyesha hivyo kuna kazi kubwa lazima itumike kwa Simba kama watahitaji kuendelea kuwa na Baleke kutokana na uwezo mkubwa alionao,” alisema kiongozi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: