Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazawa wawapoteza mbaya akina Baleke

Baleke Simba H.jpeg Wazawa wawapoteza mbaya akina Baleke

Tue, 2 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mechi 15 zimechezwa mwezi Aprili, huku wazawa wakiwafunika wageni kwa kupachika mabao 30 kati ya 40 yaliyofungwa ndani ya mwezi huku kipigo kikubwa kikiwa ni kati ya Yanga na Kagera Sugar.

Mwezi Aprili umetamatika juzi (Jumapili) na kwenye mabao hayo, mzawa Jeremiah Juma amefungana na Jean Baleke na Stephan Aziz Ki kwa kupachika mabao matatu ndani ya mwezi huo.

Juma na Baleke wamefunga mabao hayo kwenye mechi mbili tofauti huku Azizi Ki akifunga hat trick kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Baleke alifunga dhidi ya Ihefu FC mabao mawili Simba ikiibuka na ushindi wa 2-0 na aliwafunga watani zao Yanga bao moja kwenye ushindi wa 2-0 bao lingine lilifungwa na Kibu Denisi.

Wakati Juma alifunga bao moja dhidi ya Geita Gold timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1, aliifunga Ruvu Shooting mabao mawili timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Akizungumza nasi, Juma alisema anafurahi kuwa mmoja wa wachezaji wanaoipa matokeo timu yake kipindi hiki ambacho wanapambana kuibakiza timu ligi kuu.

"Sifikirii zaidi mabao ninayofunga, napambana kuhakikisha timu inapata matokeo ambayo yatatupa pointi tatu muhimu lengo ni kuona tunaendelea kucheza ligi msimu ujao," alisema.

MECHI ZILIZOCHEZWA APRILI Geita Gold vs Tanzania Prisons (1-3), Kagera Sugar vs Mbeya City (1-0), Coastal Union vs Mtibwa Sugar (1-0), Dodoma Jiji vs Kinondoni MC (1-0), Ruvu Shooting vs Azam (1-3), Polisi Tanzania vs Ihefu (2-1), Simba vs Yanga (2-0), Yanga vs Kagera Sugar (5-0).

KMC vs Geita Gold (0-2), Ihefu vs Simba (0-2), Namungo vs Mbeya City (2-1), Dodoma Jiji vs Coastal Union (1-1), Tanzania Prisons vs Ruvu Shooting (3-1), Azam vs Mtibwa Sugar (2-1) na Singida Big Star vs Polisi Tanzania (3-0)

WAFUNGAJI Jeremiah Juma (3), Dany Lyanga na Idd Nado (2), waliofunga moja ni Ramadhani Mbangula, Juma Liuzio, Edwine Balua, Collins Opare, Pius Buswita, Maabad Maulid, Raizin Hafidh, Shiza Kichuya, Kibu Denisi, Jacob Masawe, Abdulrazack Mohammed, Elius Mahuli, Gustapha Lunkombi, Geofrey Luzendeze, Jumanne Elfadhili, Valentino Mashaka, Vitalis Mayanga na Nickson Kibabage.

Kwa wageni waliofunga ni, Fiston Mayele, Aziz Ki na Baleke wote matatu, huku Pascal Wawa, Amissi Tambwe, Issa Ndala wakifunga moja kila mmoja.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: