Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajaa tu hakuna 'Sold Out' wala 'Full House' - Oscar Oscar

Mashabiki Mkapa Simba.jpeg Wanajaa tu hakuna 'Sold Out' wala 'Full House' - Oscar Oscar

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba na Yanga zimezoea kuwa na utamaduni wa kuweka takwimu za mauzo ya tiketi katika mechi hasa zile zenye ukubwa na mvuto kama vile Kariakoo Dabi ama mechi ya Kimataifa.

Bahati mbaya kwa Simba na Yanga wanaweza kuandika tiketi SOLD OUT ama FULL HOUSE alafu siku ya mchezo unakuta kuna mapengo. Sitaki kujua nini kinatokea nyuma ya hili.

Pale nchini Misri ambapo mabingwa mara 11 wa Ligi ya Mabingwa Afrika walipo yaani Al Ahly,wao hawana mambo ya full house ama Sold Out. Wenzetu kila mechi wo wanajaa tuu.

Tujifunze kwa wenzetu kuupenda zaidi mchezo wa mpira wa miguu,hapa kwetu tunapenda ila hatujapenda moja kwa moja. Zile kelele za mashabiki pale Cairo zinaweza kuwachanganya wachezaji wa Simba na kujikuta wanachezea kichapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: