Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliotemwa Simba SC waondolewa Kambini

Mwanuke Kambini Waliotemwa Simba SC waondolewa Kambini

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana Simba iliachana na wachezaji wake watano ambao haitaendelea nao na tayari imewaondoa kambini huko Zanzibar ambako timu hiyo inashiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Simba leo Jumatano itacheza mechi yake ya nusu fainali ya mashindano hayo dhidi ya Singida Fountain Gate kwenye Uwanja wa New Amaan Complex hivyo nyota hao hawatakuwepo.

Nyota hao sasa wanakwenda kuanza maisha mapya kwenye timu nyingine ambapo baadhi yao wamevunjiwa mikataba huku wengine wakitolewa kwa mkopo.

Waliotemwa ni Shaban Chilunda, Nasoro Kapama, Jimyson Mwanuke, Ahmed Feruzi na Abdallah Hamis.

Hata hivyo, kati ya wachezaji hao watano ni wanne pekee ambao walikuwepo Zanzibar, Kapama hakuwa ndani ya kikosi hicho kwani alikuwa anatumikia adhabu yake ya kusimamishwa kwa utovu wa nidhamu pamoja na Clatous Chama na tuhuma zao bado hazijasikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya Simba.

Madai ya Kapama yalidaiwa ni kushindwa kuhudhuria mazoezi akishinikiza kuondoka ili akatafute changamoto mpya sehemu nyingine kwani ndani ya Simba hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Chilunda na Abdallah wamesajiliwa msimu huu hivyo wamekaa ndani ya Simba nusu msimu Mwanuke amekuwa Simba kwa miaka mitatu, Feruzi alipandishwa kutoka U20 na Kapama amekuwa na mwaka wa pili. Na wachezaji wote hawa walikosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

"Huku kambini wameondolewa baada ya kupewa hizo taarifa, wengine wameenda kwa mkopo na wengine wamevunjiwa mikataba," alisema kiongozi mmoja wa Simba ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: