Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Yanga: Simba wamemdharau sana Mwenyekiti Mangungu

Simon Patrick X Samia Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick awapa Simba somo

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumapili iliyopita Simba walikuwa na Tamasha lao la "Simba Day" katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kilele cha Tamasha hilo kilifana sana huku Simba wakipongezwa na wadau mbalimbali wa soak kwa namna walivyofanikisha Tamasha hilo.

Mgeni Rasmi katika Tamsha hilo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Miongoni wa watu waliotoa pongezi zao ni Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga wakili Simon Patrick ambae kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alinogesha sherehe yenu watani hongereni, ila siku nyingine rekebisheni protocol, Mwenyekiti wa Klabu Mzee Mangungu sio wa kukaa VIP A, alipashwa akae hapo na mgeni rasmi kwani yeye ndio Kiongozi wa juu kwenye Klabu.

Je unakubaliana na kauli na ushauri huo wa Wakili Simon Patrick? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: