Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji wa Simba wafungiwe ndani na ulinzi mkali kama jeshini - Shabiki

Simba Kikosi Kwenda Misri Wachezaji wa Simba wafungiwe ndani na ulinzi mkali kama jeshini - Shabiki

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, maarufu kwa jina la Mchome amesema kuwa uongozi wa klabu hiyo unapaswa kufanya maamuzi magumu ya kuwaweka kambini wachezaji wa timu hiyo na kuwaondolea uhuru wa kutembea mitaani hovyo, kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kurejesha heshima, kuzingatia ratiba na kurejesha utimamu wa miili yao kuelekea michuano iliyoko mbele yao.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kuwa na matokeo mabovu ambapo katika mechi tatu za mwisho haijashinda hata mchezo mmoja na ikikumbukwa kuwa imetoka kutoa sare na ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

"Wamekaa muda mrefu na kikao kirefu sana, nadhani walikuwa wanajadili mwenendo wa matokeo tunayoyapata na sidhani kama wamepata jibu sahihi. Mimi naweza kuwasaidia kuwa tatizo ni wachezaji hawakai sehemu moja.

"Wachezaji wa Yanga wanakaa kambini Avic Town lakini wachezaji wa Simba hawajulikani wanaishi wapi. Bunju hakuna makazi ya watu. Wachezaji wa Simba wamesambaa, wengine wameoa, wanaishi na mademu, viongozi hawawezi kujua.

"Anaweza kumuita binti akajifungia nae hata wiki mbili, fitness level yake lazima ishuke. Cha kwanza wawafungie wachezaji wote kambini kama jeshini na ulinzi mkali hakuna mtu kutoka. Kuna wakati wanachelewa kulala au wanakula vyakula ambavyo si sahihi.

"Kingine wapewe mazoezi magumu kuliko mechi ili kurejesha fitness level yao, vitambi vipungue, wamelegea sana. Wapangiwe muda wa kulala, muda wa kuamka, muda wa kula, aina ya chakula, watu wa kukutana nao, simu zao zikamatwe mpaka makundi yaishe uone kama Simba hatutatonoa makundi," amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: