Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji hawa Simba viwango vyao vitaporomoka - Oscar Oscar

MOHAMED MUSSA Wachezaji hawa Simba viwango vyao vitaporomoka - Oscar Oscar

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imekuwa kama Manchester United hasa kwa wachezaji wazawa ambao wamekuwa wakisajiliwa kila msimu na baada ya msimu mmoja wanandoka hao wachezaji ama wanakufa viwango.

Tatizo ambalo naliona kwa Simba ni kwamba kile kizazi chao cha dhahabu cha misimu minne tayari kimeshaisha makali na wachezaji umri umekwenda ila bado wanaendelea kuchezesha hao hao.

Kuna wachezaji kama Nasoro Kapama, Jimmyson Mwanuke, Mohamed Mussa hawa wapo tu pale kikosini kujaza idadi ya wachezaji wa mazoezini. Angalia moto aliokuja nao Yusuph Mhilu ila ameondoka kiwango chake kimeshuka.

Hata hawa ambao wamesajili msimu huu hakuna ambaye amepata nafasu zaidi ya kucheza mechi za Kirafiki. Kama Simba hawatawaamini hawa vijana na kuwapa nafasi basi itakuwa kama Manchester United inavyoua viwango vya wachezaji wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: