Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vunja Bei atoa kauli ya Shukrani Simba SC

Fred Aishukuru Simba Vunja Bei atoa kauli ya Shukrani Simba SC

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurungezi wa Kampuni ya Vunjabei Fred Ngajilo ametoa Shukrani kwa Klabu ya #SimbaSportsClub kwa kumuamini na kufanya nae kazi kwa Miaka Miwili huku akisema kuwa wameleta mapinduzi makubwa kwa Tasnia ya Utengenezaji na usambazaji wa Jezi na vifaa vya Michezo, Kupitia ukurasa wake wa Instagram #Fred ameandika....

"Verified Menejimenti ya Vunjabei (T) Group Limited inapenda kutoa shukrani za dhati kwa bodi ya wakurugenzi, menejimenti, benchi la ufundi, wachezaji, wanachama na mashabiki wote wa Simba Sports Club kwa ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakitupa katika kipindi chote cha miaka miwili ambayo tumefanya kazi ya Mapinduzi makubwa ya tasnia hii ya utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya michezo.

Tunatarajia kuendelea kudumisha uhusiano huu tulioujenga, tunachukua fursa hii kumpongeza mzabuni mpya na hatutasita kumpa ushirikiano wa aina yeyote pale tutakapohitajika.

Tunaamini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuelekea kwenye mafanikio zaidi na kusababisha maendeleo katika mpira wetu wa miguu Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: