Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya Bocco na mashabiki inatoka wapi?

Bocco Pic Vita ya Bocco na mashabiki inatoka wapi?

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwenye mchezo wa mpira mashabiki wana vigezo viwili kushabikia kwa furaha na kushabikia kwa kuzomea hakuna namna nyingine ya kumbadilisha mshabiki maana yeye ndiye uchagua wakati huu atatumia njia ipi ya kushangilia.

Wazungu wanasema TOO MUCH IS HARMFUL (Kupita kiasi kuna madhara) imekuwa sasa vita ya mashabiki juu ya John Bocco inaonekana ni dhambi kubwa kuwepo Simba mpaka sasa.

Ukitaka kuona vita hii ni pale klabu ya Simba inapo post picha za John Bocco comment nyingi sana ni kejeli na matusi tu huku ukijiuliza kuna tukio kafanya la timu kukosa ushindi uonii.

Pia kipindi cha pili John Bocco alipoingia niliona kitendo ambacho siyo cha uungwana baada ya John Bocco kukosa bao pasi kutoka kwa Chama. Mashabiki walianza kumrushia chupa za maji huu siyo ushabiki kwa wapenda mpira, kitu cha ajabu hao hao mashabiki walifurahi tena goli ambalo alisababisha wapinzani kujifunga.

Mpaka najiuliza ndio huyu John Bocco ambaye misimu minne nyuma alikuwa anaimbwa na mashabiki kila kona kwa ufungaji wake wa mabao huyu si ndio Bocco amepambana timu mpaka kuchukua mataji manne ya ligi kuu, FA na kucheza robo fainali 4.

Kuna msemo usema kama huwezi kumsaidia mtu ni kheri kukaa kunyamaza kuliko kuongea. Kama inaonekana John Bocco kwako hafai haina umuhimu wowote wa kumtupia maneno ambayo mengine siyo mazuri ambayo kama mchezaji na binadamu hayawezi kumfurahisha kwa namna yoyote ile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: