Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wababaishaji wanavyoitesa Simba SC soko la usajili

Beno Mcameroon Viongozi 'Wasanii' ndio wanaoitesa Simba katika usajili

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Mkataba wa Beno Kakolanya na Simba SC Ukielekea mwisho baadhi ya Viongozi walimuita na kuketi nae Chini ili kuanza mazungumzo nae juu ya kuongeza Mkataba mpya.

Uongozi wa Simba ulitaja ofa yao kuwa upo tayari kumpa kiasi cha Tsh.45 Milioni kwa miaka miwili (2) na Mshahara wa Tsh. 4 Milioni.

Wakati ofa yake Yeye Beno kakolanya alikuwa akihitaji Tsh. 65 Milioni kwa Miaka Miwili na Mshahara wa Tsh. 6 kwa Mwezi.

Uongozi wa Simba Sc uligomea na kusema ni kubwa sana kwake na hautakuwa tayari kumpatia hiyo,

Beno Kakolanya alifikia maamuzi ya Kuachana na Mazungumzo na Waajiri wake hao na kuamua kusikiliza klabu itakayokuja mbele yake.

Azam Fc ndiyo ilikuwa klabu ya kwanza na Walimpa ofa yao huku Singida Fountain gate nao wakiweka mezani ofa yao.

Beno aliamua kujiunga na klabu ya Singida kutokana na ofa yao kuwa bora zaidi kwa upande wake. Ada ya usajili wa Miaka miwili wakimtengea Tsh. 100 Milioni kwa miaka miwili na Mshahara wa Tsh.6 Milioni kwa mwezi, kitu ambacho hakupinga kabisa.

KIPA MPYA NDANI YA SIMBA NA DAU LAKE.

Kwasasa Kama mambo yakienda kama yalivyopangwa kipa Mcameroon, Simon Omossola (25) anaweza kusaini Simba muda wowote,

Inafahamika dhahiri kuwa Simba imeachana na dili la kipa Mbrazili Caique da Santos kwa sababu mbalimbali ikiwemo kigezo cha kutoridhishwa na Kiwango chake lakini kwa sasa wapo siriazi na Omossola aliyesaini miaka miwili na FC Saint Eloi Lupopo Krismasi iliyopita,

Tunafahamu kuwa mezani kwa Simba yamebaki majina ya makipa wawili moja ni wa Lupopo aliyetoka AS Vita ya DR Congo, Omossola na lingine ni la Mbrazil mwingine aliyependekezwa na kocha Robertinho baada ya dili la Caique kukwama,

Hata hivyo, Omossola anaonekana kupigiwa chapuo na viongozi wengi wa jopo la usajili hivyo wakiafikiana huenda akawa mbadala wa Beno Kakolanya na atakayeziba pengo la Aishi Manula anayeuguza majeraha hadi Mwezi Novemba,

Simba Sc inaamini uzoefu wa Omossola katika mashindano ya Afrika na timu ya taifa ya Cameroon vitaisaidia kufikia malengo,

Inafahamika Simon Omossola dau lake linatajwa si chini ya TSh.400 milioni kwa Miaka Miwili huku Mshahara wake ni zaidi ya Tsh.10 Milioni kwa Mwezi.

Je Mwanasimba viongozi wetu wanapatia ama wanakosea? kama wangempa Beno alichohitaji suala la Golikipa lingekuwa ni habari mpya hii leo? Tuachie maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: