Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi Simba ni kama wanakimbia kivuli chao

Kocha Abdelhak Benchikha Kocha Abdelhak Benchikha

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa Simba wanajificha kwenye kivuli cha walimu,lakini haya ni matokeo ya uongozi wao dhaifu.

Madirisha manne mfululizo wamekwama kufanya usajili wa maana wakati huo Mkude, Kagere, Onyango, Wawa, Mugalu na Bwalya wameondoka pasipo kupata mbadala wao sahihi.

Tunawasema Chama, Saido, Kapombe na Zimbwe wamechoka lakini tukumbuke hawa ni binadamu wametumika mno bila mapumziko miaka yote wanatumika wao kwasababu sajili mpya hazifanyi vizuri.

Hii leo mashabiki wameanza kugoma kuingia uwanjani matokeo yake uchumi wa timu utashuka.

Kila siku Viongozi wanajificha nyuma ya mgongo wa makocha na kwa hali hii hata Ben Chikha ana kazi ngumu mbele ya hili kundi la hawa wachezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: