Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Video analyst aomba kazi Simba

Video Analyst Alexandre Kerveillant

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa mtathmini wa video na viwango wa Klabu ay Al Nassr ya Saudi Arabia ambayo kwa sasa anachezea Cristiano Ronaldo, Alexandre Kerveillant amewasilisha maombi mezani kwa Simba SC akitamani kupewa kazi hiyo ambayo kwa sasa inafanywa na Mzimbabwe, Culvin Mavunga.

Baada ya kupata fununu kuwa Simba SC kwa sasa inafanya tathmini ya utendaji kazi wa Mavunga kuona kama imfungulie milango au ibaki naye,

Kerveillant amewasha kompyuta yake mpakato ‘Laptop' fasta kisha akatupa barua pepe kwa uongozi wa Simba SC akiwapa wasifu wake mrefu unaoonyesha uzoefu wa kutosha alionao wa kazi hiyo.

Kerveillant ambaye pia ni kocha mwenye leseni ya juu umoja wa vyama vya mpira wa miguu Ulaya ‘UEFA’, miezi miwili iliyopita aliachana na Nantes inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa ambayo alikuwa akiitumikia katika majukumu hayo akimsaidia Antoine Kombouare.

Mfaransa huyo ana wasifu ulioshiba wa kazi ya kutathmini viwango na video kwenye timu na ushuhuda wa hilo ni timu ambazo amewahi kuzifanyia kazi kwa nyakati tofauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: