Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukuta wa Yeriko unapasuka vipande vipande

Che Malone 966688 Ukuta wa Yeriko unapasuka vipande vipande

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mlinzi wa kati Che Malone Fondoh akisajiliwa pale Simba SC, mashabiki wa timu hiyo waliamini kwamba watakuwa na safu bora ya ulinzi kuliko hata timu zote.

Furaha ya mashabiki wa Simba ilienda mbali baada ya Che Malone kupewa jina la Ukuta wa YERIKO, walifananisha ile stori kuhusu huo ukuta wa Yeriko na wakaona sasa hakuna shida pale nyuma, Babu Onyango asepe tu.

Katika mechi tatu ambazo Simba wamecheza pale nyuma ambapo alikuwa akicheza Che Malone Fondoh na wenzake wamefungwa magoli manne hadi sasa. Mawili Liggi Kuu na mawili Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.

Hadi sasa ukuta wa YERIKO unaendelea kupasuka chini ya Hennock Inonga, Che Malone na wenzake.

Kama wasipokuwa makini basi Simba itakuwa inapitia wakati mgumu kwa makipa wake kupata, inabidi mwalimu Robertinho akae na mabeki wake waone namna ya kuyafanyia kazi mapungufu yao.

Ni sahihi kabisa kila timu inafungwa duniani, hakuna timu isiyofungwa, lakini kuna kila sababu ya kupunguza makosa kwani zipo mechi au mashindano ambayo yataamriwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo ni vyema sasa kuweka mfumo mzuri wa Simba kujilinda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: