Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchambuzi wa George Ambangile; Simba vs Tanzania Prisons

Chama Jmk Simba vs Tanzania Prisons

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: George Ambangile

"KOPLO SAMSON MBANGULA .! ⚽️⚽️

Nafikiri kocha mzuri anayefanya homework kujua nguvu ya mpinzani na mapungufu yake, Ahmed Ally kocha wa Tanzania Prisons alichofanya.

1: Dhidi ya Simba hutakiwi kuwa na abiria uwanjani, lazima uwe na watu wanapambania mipira, wanakimbia zaidi, lakini ukitembee, ukisinzia, ukiwapa muda na nafasi kwenye mpira basi kipo ambacho utakipata kibaya.

2: Kwenda mbele jitahidi uwe na watu wenye kasi, Simba wakishambulia mara nyingi fullbacks wao huwa wanasogea juu zaidi (huwa wana imani na mabeki wao wa kati kukabiliana na counter attacks) kwahiyo ukiwa mfanisi utapata chochote kitu

Kiufupi: Zuia vizuri kwenye mita zako 30 za mwisho halafu shambulia vizuri kwenye transitions.

Nafikiri leo Simba badala ya kusema wapi walikosea cha kwanza ni kuwapongeza Prisons jinsi walivyofanya kazi uwanjani ... yes kuna nyakati walikuwa slow sana wachezaji wao kufanya maamuzi sahihi kama:-

1: Kufanya runs mbele ili kumpa options mwenye mali

2: Kupiga pasi haraka badala yake mchezaji anakaa na mpira muda mrefu

3: Sehemu yenye kuhitaji utulivu " baadhi " yao walikuwa na maamuzi ya haraka : kama sehemu ya pasi mtu anauma meno kushuti.

NOTE

1: Nafikiri goli la kwanza hesabu za Manula zilimpoteza ile touch ya mwisho ya Mbangula ilikuwa ndefu sana pengine Manula angeweza ku sweep

2: Yona: amenivutia huyu kipa leo: Sehemu ya kudaka krosi anafanya hivyo , sehemu ya kupanchi anafanya hivyo, yupo active sana kuhusika na mchezo hasa sweepings nyuma ya walinzi wake.

3: Nafikiri sehemu ambayo kocha wa Prisons atakuwa anashukuru ameshinda licha ya maamuzi yake ni kumtoa Samson Mbangula... baada ya pale mipira ilikuwa haikai mbele na ni mtu alikuwa anawafikirisha sana walinzi wa Simba.

4: Mipira iliyokufa Ngoma huwa anakuwa active sana anaijulia mno

5: Mbangula... a centre forward performance. Kucheza mbele peke yako sio rahisi aisee!

FT: Simba 1-2 TZ Prisons"

Chanzo: George Ambangile
Related Articles: