Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshabalala ni zaidi ya Nahodha pale Msimbazi

Tshabalala X Kapombe Mo Tshabalala ni zaidi ya Nahodha pale Msimbazi

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mchezo wa Dabi ya Kariakoo ukiendelea Kuna muda nilikuwa namtazama Tshabala kwa jicho la huruma sana.

Alikuwa anapambana na watu wawili hatari sana. Yao Kouassi na Pacome. Kuna wakati Maxi na yeye alienda upande wake.

Bahati mbaya alikuwa upande mmoja na Chama ambaye hapendi kuzuia na si mkabaji mzuri. Unaweza kuelewa Tshabalala alikuwa anapitia nini uwanjani.

Baada ya bao la nne la Maxi, wakati wenzake wengi wamekata tamaa mioyo imekufa, yeye bado alikuwa anaamini wanaweza kufanya kitu kuzuia aibu iliyokuwa mlangoni kwao. Nilimuona akikazana kuwahamasisha wenzake,, bahati mbaya sio wote walikuwa na uchungu na timu kama yeye.

Hali aliyokuwa nayo baada ya mchezo.. Ulihitaji moyo wa chuma kuthubutu kwenda mbele ya camera kufanya mahojiano kwa niaba ya timu nzima..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: