Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshabalala na Mkataba mnono alioustahili Simba SC

Tshabalala Simba Mlinzi wa Simba, Mohamed Hussein "Tshabalala"

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nimesoma mahala Mohamed Hussein ‘ Tshabalala’ amesaini mkataba mpya wa miaka miwili Msimbazi. Haishitui.

Nasikia ni mkataba mnono. Kiufupi tu, huo ni mkataba alioustahili. Ndani ya uwanja Tshabalala ana nidhamu. Nje ya uwanja ana nidhamu pia.

Tuna wachezaji wachache wenye nidhamu yake kuanzia wachezaji wa kizawa au hadi wale wa nje.

Wengi nidhamu zao ni za kuigiza. Wengi ukiwaambia kitu kuhusu nidhamu wanajua unamaanisha kuamka asubuhi na kusema Shikamoo kocha.

Katikati ya kundi la mastaa wa kimataifa pale Simba, Tshabalala ni moja ya staa wa kizawa aliyeamua kula sahani moja na mastaa wa kimataifa.

Mastaa wengine wa ndani wamejifia kifo cha kawaida, kabisa, hawaonekani wala hawafurukuti, lakini Tshabalala anapambana nao. Hii sio kitu cha kawaida.

Nafasi nyingi za wachezaji wazawa siku hizi zimekwenda kwa mastaa wa nje, kina Tshabalala wachache wanapambania nafasi. Good.

Kila zinapowekwa sheria za kuruhusu ongezeko la wachezaji wa kimataifa, nafasi za wazawa zinazidi kuwa hafifu. Itafika muda wanaume 11 wa timu zetu zitakuwa na sura wa wageni.

Tunapoona kina Tshabalala wanapambana na wageni sio bahati mbaya, wanawakilisha kundi kubwa la wachezaji wa kizawa lililojifia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: