Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Try Again afunguka ishu ya Sven Simba

Sven Vandenbroeck Ms Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Sven Vandenbroeck

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdalla ‘Try Again’ amesema ni kweli Simba inasaka kocha lakini watawatangazia mashabiki wao watakapompata kocha sahihi.

Akizungumzia suala la kocha wakati akihojiwa katika kituo cha Azam TV baada ya kutajiwa jina la Sven Vandenbroeck alisema ni kocha mzuri aliacha rekodi nzuri ndani ya Simba na amefanya mambo makubwa Morocco.

“Ni kocha mzuri lakini siwezi kusema ndiye anayeweza kuja kuinoa Simba ila mashabiki na wanasimba wanatakiwa kufahamu tutamleta kocha mzuri anayelifahamu soka la Afrika na Ligi ya Mabingwa;

“Lengo ni kuona anatuongoza kuanzia tulipo na kutufikisha sehemu kubwa ambayo tumekuwa tukiitamani muda mrefu hatua ya Nusu fainali Ligi ya Mabingwa na mchakato wake unaenda vizuri anaweza kuja kabla ya mchezo wetu wa hatua ya makundi nyumbani au baada,” alisema Try Again.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: