Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Try Again: Tunaenda kupindua meza ugenini

Try Again Usajili Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’

Sat, 30 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya jana usiku Simba kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka Al Ahly mchezo wa mkondo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bado Simba hawajakata tamaa katika kuhakikisha wanasonga mbele hatua ya nusu Fainali huku wakiahidi kufanya maajabu katika mcheo wa mkondo wa Pili nchini Misri.

“Bahati haiwezi kuwa kwao kila siku, leo imekuwa bahati kwao, kesho inaweza kuwa kwetu, cha msingi kuwa na morali, umoja, upendo na kujiandaa, hatuwezi kwenda kushinda ugenini kama tutakata tamaa. — Mwenyekiti wa Bodi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’

“Mimi naamini kwa timu tuliyonayo, kwa nyinyi mlivyo mimi naamini kabisa tunaenda kupata ushindi, tusikate tamaa hata kidogo morali yetu iwe juu kabisa kupita hii tuliyokuwa nayo mimi naamini mnaweza kufanya hivyo na tukapata ushindi ugenini.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: