Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Try Again: Tumeshamaliza kila kitu, wachezaji washindwe wao tu

Try Again 01 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdallah "Try Again"

Wed, 3 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdullah 'Try Again' amewatoa hofu mashabiki waliokata tamaa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Machi 29, 2024

Try Again amesema nafasi ya timu hiyo kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo bado ipo kwani wana dakika nyingine 90 za kupambana na kupata matokeo mazuri.

"Sisi tupo mawindoni, hatuwezi kukata tamaa ndio maana kuna mchezo wa kwanza na wa pili, tuna nafasi nyingine ya kupambana na tumejiandaa vizuri."

Ameongeza kuwa, wachezaji wamepewa motisha kubwa ili kuongeza morali ya kupambana kupata matokeo mazuri.

"Tumewapa motisha kubwa, Rais wa Heshima, Mohamed Dewji ameweka motisha kubwa ambayo haijawahi kutokea, nisingependa kuweka wazi, wachezaji washindwe wenyewe."

Try Again amesafiri na timu kwenda Cairo kwaajili ya mchezo wa pili wa robo fainali ya CAFCL utakaochezwa April 5, 2024 kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo saa 5:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

View this post on Instagram

A post shared by Mwanaspoti (@mwanaspoti_tz)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: