Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Try Again: Infantino ameniambia Simba inacheza mpira mzuri kuliko Mamelodi, Wydad

Try Again X Infantino Try Again: Infantino ameniambia Simba inacheza mpira mzuri kuliko Mamelodi, Wydad

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salim Abdallah maarufu kama "Try again" amesema soka linalochezwa na Klabu ya Simba ni la kiwango cha juu kiasi ambacho mpaka viongozi wa ngazi za juu FIFA wametoa pongezi.

Try Again ambae alipata wasaa wa kuhudhuria mchezo wa Mkondo wa pili wa Fainali ya Michuano ya African Football League nchini Afrika ya Kusini Jumapili iliyopita kati ya Mamelodi na Wydad alikaa jukwaa moja na viongozi wa Juu wa CAF na FIFA.

Akizungumza kupitia kituo cha Televisheni cha Azam TV, Try Again amesema;

"Juzi wakati nipo V.I.P Kiongozi wa FIFA aligeuka na kuniambia timu yako (Simba SC) inacheza vizuri kuliko timu zinazocheza hapa (Mamelod Sundowns na Wydad kwenye Fainali ya AFL )"

Msikilize kwa Urefu akizungumza hapa chini;

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: