Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu zote zilizofuzu nusu fainali CAFCC hizi hapa

Aziz 630471 Aziz Ki

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga wemeweka historia ya kutinga kwa mara ya kwanza hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Rivers United kwa jumla ya mabao 2-0 ambayo waliyapa kwenye mchezo wa kwanza nchini Nigeria kabla ya kutoka suluhu kwa Mkapa.

Vijana hao wa Nasreddine Nabi watacheza dhidi ya Marumo Gallants F.C. ya Afrika Kusini kwenye hatua ya nusu fainali.

Timu zilizotinga nusu fainali kombe la Shirikisho Afrika

Yanga SC - Tanzania Asec Mimosas - Ivory Coast USM Alger - Algeria Marumo Gallants - Afrika Kusini

Droo ya nusu fainali CAFCC

Yanga SC vs Marumo Gallants

Asec Mimosas vs USM Alger

Yanga wataanzia nyumbani katika Uwanja wa Benjamin Mkapa mnamo Mei 10, 2023 kabla ya kurudiana na Marumo Gallants huko Afrika Kusini wiki moja baadae Mei 17, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: