Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha USM Alger aichimba mkwara Yanga

Abdelhak Benchikha.jpeg Kocha Abdelhak Benchikha

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa UCM Alger ya Algeria, Abdelhak Benchikha amesema hana hofu na kiwango cha Yanga na wategemee mechi ngumu zaidi ya zote zilizopita kwani wanahitaji kombe hili.

"Wanatakiwa kufahamu kuwa wanakwenda kukutana na timu ya tofauti kuliko walizokutana nazo katika hatua waliyocheza,tunalihitaji hili kombe,tunaheshimu uwezo wao," Kocha USM ALGER, Abdelhak Benchikha.

Yanga atakutana na USM, Jumapili ijayo, Mei 28, 2023 katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa katika Dimba la Mkapa jijini dar es Salaam na mchezo wa pili utapigwa Algeria Juni 3.

USM ALger imetinga fainali ya michuano hiyo kwa kuiondoa AS FAR Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 4-3 huku Yanga ikiiondoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: