Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetesi: Simba kuachana na Saido

IMG 4294 Saido.jpeg Tetesi: Simba kuachana na Saido

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Saidi Ntibazonkiza anamaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi mwishoni mwa msimu huu na atakuwa Mchezaji huru (Free agent) ambapo Simba haifikirii kumuongezea mkataba.

Taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Simba zinasema kuwa uongozi wa timu hiyo na wawakilishi wa Saidi Ntibazonkiza haijafikia makubaliano ya kumuongeza mkataba, inatajwa kuwa Wekundu wa Msimbazi watamuachia Mchezaji kuondoka ila wataangalia mustakabali wake dirisha lijalo la usajili.

Kuna taarifa za chini chini kuwa Simba inaonekana haina mpango wa kuendelea kupata huduma ya Saidi Ntibazonkiza kwa muda mrefu zaidi, inatajwa Wekundu wa Msimbazi wataachana na mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: