Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Makamu Mwenyekiti wa zamani Simba SC afariki Dunia

Mwenyekiti Wa Zamani Simba.jpeg Fakhruddin Amijee

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba SC miaka ya 1990, Fakhruddin Amijee amefariki dunia jana jioni nyumbani kwake Arusha akiwa ana umri wa miaka 84 baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mfupi .

Amijee aliyewahi pia kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Dar es Salaam (TAREVA) na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanzania (TABA) amezikwa jana hiyo hiyo usiku Jijini Arusha.

Amijee alikuwa Makamu Mwenyekiti Simba kuanzia mwaka 1990 chini Mikidadi Kasanda, Juma Salum baadaye chini ya Ally Amir ‘Bamchawi’ na Priva Mtema (wote marehemu) mwaka 1996 na baada ya hapo akahamia kwenye michezo mingine na kuongoza TAVA na TABA.

Enzi za uhai wake marehemu Amijee alikuwa kiongozi wa msafara wa mechi zote za ugenini Simba wakifika Fainali Kombe la CAF mwaka 1993.

Lakini pia atakumbukwa kwa kuileta klabu ya Stoke City ya England ambayo ilicheza mechi za kirafiki na timu za Simba, Yanga Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Coastal Unión Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Amijee ameacha mke, Sukaina na watoto watatu, Zahra, Husain na Zainab.

Mungu ampumzishe kwa amani. Amín.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: