Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa mpya Simba huyu hapa

Ladack Chasambi Vv Kiungo wa Mtibwa Sugar Ladack Chasambi

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Muda wowote kuanzia sasa, Simba itamtangaza kiungo mshambuliaji, mpya, Ladack Chasambi aliyesajiliwai kutoka Mtibwa Sugar.

Kinda huyo aliyekuwa mchezaji bora ndani ya miaka miwili mfululizo kwenye Ligi ya Vijana (U-20), alipandishwa na Mtibwa rasmi msimu huu, ingawa huko nyuma walikuwa wanampa nafasi ya kucheza mara moja moja kikosi cha wakubwa.

Kiwango chake kiliwashawishi viongozi wa Simba kumsaini miaka mitatu, ili kuongeza nguvu safu yao ya ushambuliaji na kuona watamtumia kwa muda mrefu.

Kuna baadhi ya mashabiki walikuwa hawaamini kama Chasambi kasajiliwa, leo watapata uhakika wa kumpokea mchezaji wao mpya.

Ndani ya kikosi cha Simba kuna viungo washambuliaji kama Said Ntibanzokiza 'Saido', Clatous Chama, Kibu Denis hivyo atakuwa na wakati wa kujifunza uzoefu kutoka kwao na akifanya bidii, atamwamini kocha kumpanga kikosini.

Usajili wake umemuibua straika wa zamani wa Mtibwa, Abdallah Juma alisema Chasambi ana uwezo mkubwa sana, anachotakiwa kukifanya ndani ya Simba ni kuonyesha nidhamu ndani na nje ya uwanja.

"Anajiunga na timu ambayo ina ushindani wa namba, ila kwa uwezo wake namwamini, jambo la msingi ni mchezaji kufanya bidii kuwaonyesha hawakukosea kumsajili, mtulivu, hana mambo mengi, aendelee hivyo asije akabadilika anapofika mjini," amesema

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: